kocha Mkuu wa timu ya taifa ya England,Roy Hodgson
amesema atasubiri kuona kama ataweza kumuita kwa mara nyingine beki wa
Manchster United Rio Ferdinand.
Kocha huyo amesema alijisikia vibaya kuona
Ferdinand akijiondoa kwenye timu ya taifa ya England baada ya kumuita
kwaajili ya michezo ya kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia dhidi
ya visiwa vya San Marino na Mentengro.
Ferdinand
ambaye alijiondoa kwenye kikosi hicho cha Uingereza kwa sababu za kuwa
alikwishajipangia ratiba maalumu kwaajili ya kuuguza majeraha yake
katika kipindi hiki ambacho klabu yake itakuwa haina mechi zozote kwa
zaidi ya wiki moja.
Nyota huyo wa Manchester United mwenye umri wa
miaka 34,amekwishaicheza Uingereza michezo 81 na tayari yupo nchini
Qatar tayari kwaajili ya kuwa mchambuzi kwenye mechi kati ya Uingereza
na San Marino Ijumaa hii.
Hata hivyo kocha Hodgson akijibu swali kuhusiana
na Ferdinand kusafiri hadi Qatar kuchambua mechi ambayo angekuwa
uwanjani akicheza,alisema hakuwa na wazo lolote,lakini amejisikia vibaya
kuona beki huyo hajajiunga na timu yake na kusafiri kwake kwenda Qatar
ni matakwa yake binafsi na klabu yake.
Mechi ya mwisho Ferdinand kuichezea England
ilikuwa dhidi ya Uswis mwezi Juni mwaka 2011,Alikosa fainal za mataifa
barani Ulaya mwaka 2012 ambapo kocha Roy Hodgson alisema ameacha kumuita
nyota huyo kwa sababu za Kimpira.
Hivi sasa Hodgson itamlazimu kumchagua beki wa
Manchester City Jeleon Lescott, Chris Smalling wa Manchester United ama
Steven Caulker wa Tottenham au Steven Taylor wa Newcastle United kwenye
safu ya ulinzi itakayocheza na visiwa vya San Marino Ijumaa hii katika
mchezo wa kundi H kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia mwakani
nchini Brazil.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni