Jumamosi, 23 Machi 2013

Mshichana Pakistan aliyejifanya kuwa mvulana

Maria Toorpakai WazirMaria Toorpakai Wazir

Maria Toorpakai Wazir, mshichana kutoka Waziristan, Pakistan, ambaye kwa miaka kadhaa ilibidi acheze mchezo wa squash akiwa anajidai kuwa mvulana, sasa amekuwa mchezaji shupavu.
Eneo la Waziristan ni eneo ambapo itikadi za Kiisilamu zinafuatwa sana. Kwa hivyo kwa Maria kucheza squash ni jambo la ajabu katika eneo ambalo wasichana hawakubaliwi hata kwenda shule.
Lakini Maria anasema, "Mimi ni jasiri. Nilizaliwa jasiri na nitakufa jasiri."
Babake amemuunga kwa dhati Maria kwa kumpa nafasi ingawaje anasema: "Huku kwetu wasichana hawakubaliwi hata kutoka nje wanamoishi."
Kaptula
Squash ni mchezo unaopendwa sana nchini Pakistan. Wanawake pia huucheza, ingawaje siyo eneoni Waziristan au kwenye maeneo mengine yenye itijadi kali.
Toorpakai anasema alipoanza kucheza squash akiwa kavaa kama mtoto wa kiume, si wengi waliogundua kuwa ni msichana. Lakini walipofanya hivyo walianza kumkejeli na kumtukana, lakini hakufa moyo.
Asema babake: "Wakati watu walipomuona Maria na kugundua kwamba alikuwa havai hijab, na kwamba alicheza squash akiwa amevaa kaptula, walishangaa sana na kunilaumu vikali."
Onyo
Barua ilibandikwa kwenye gari lake baba huyo lililomwambia amwachishe mwanae kucheza squash kwa sababu "ilikuwa ni kinyume na itikadi za Kiisilamu na za kabila".
Walimwambia “angeona cha mtema kuni” iwapo asingefanya hivyo.
Lakini alisisitiza kwamba kama watoto wake wa kike walikuwa na shauku la kucheza mchezo wowote ule basi yeye angewaunga mkono.
Baadaye Maria alijitahidi kutafuta mdhamini na akalekea mafunzoni Canada. Kwa sasa ndiye mchezaji wa juu zaidi wa kike nchini Pakistan, na namba 49 duniani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni